ActionAid is a global movement of people working together to further human rights and defeat poverty for all.

Kongamano la Kimataifa la Bio-Teknolojia Linatoa Wito wa Kuzuiwa kwa Muda Vyakula Vitokanavyo na Mimea Iliyobadilishwa Vinasaba

Kongamano la Kimataifa la Usalama wa Chakula linatoa wito kwa Serikali kuahirisha mipango ya kusambaza teknolojia inayotumia Mimea/Wanyama Waliobadilishwa Vinasaba (GMO) kote nchini Tanzania. Kongamano hilo linatafuta kujua kwa nini jamii duniani kote zinakataa mazao na vyakula vinavyotokana na Mimea/Wanyama Waliobadilishwa Vinasaba, na zinapigania haki za wakulima na walaji kwa kuchagua wanataka kulima mazao gani na wanataka kula nini.